MMASWALI YA SAYANSI MADA ZA DARASA LA SABA

DeogratiusMvati 565 views 13 slides Feb 15, 2025
Slide 1
Slide 1 of 13
Slide 1
1
Slide 2
2
Slide 3
3
Slide 4
4
Slide 5
5
Slide 6
6
Slide 7
7
Slide 8
8
Slide 9
9
Slide 10
10
Slide 11
11
Slide 12
12
Slide 13
13

About This Presentation

MWONGOZ WA MASWALI YA SAYANSI KWA MADA ZA DARASA LA SABA


Slide Content

1.Kuna aina ngapi za usalama katika mazingira? 4 nne
2.Taja aina 4 za usalama
I.Kuzuia au kukataza
II.Onyo au tahadhari
III.Lazima au amri
IV.dharura
3.Alama za usalama katika mazingira huwasilishwa
kwa kutumia nini? Rangi na umbo maalumu
4.Alama za usalama katika mazingira zimeanzishwa
kwa kuzingatia nini? Taratibu za kiusalama za
kimataifa
5.Alama za kukataza katika mazingia huwasilishwa
kwa kutumia rangi gani? nyekundu
6.Alama gani ya usalama katika mazingira
huwasilishwa kwa kutumia rangi nyekundu? Alama
za kukataza
7.Alama gani ya usalama katika mazingira inatoa
maelekezo
ya,hatari,simama,zima,hama,hairuhusiwi kuingia
kwa asiyehusika? Alama ya kuzuia au kukataza
8.Alama gani ya usalama katika mazingira inatoa
maelekezo ya kutokuruhusiwa mahali pasipo
kuhusu. Alama ya kuzia au kukataza
9.Amina alipofika chumba kile kabla ya kuingia aliona
alama iliyomuelekeza haruhusiwi kuingia katika
chumba hicho je hiyo alama amina aliyoinoa ni
alama gani? alama ya kuzuia au kukataza
10.Alama ya usalama katika mazingira ya kuzuia au
kukataza inawakilishwa kwa kutumia umbo gani?
Duara,pembe nne,picha nyeusi kwenye msingi
mweupe na kingo nyekundu,na baadhi ya alama
zina mstari mwekundu wa kiegema.
11.Alama za usalama katika mazingira za kukataza
linawakilishwa kwa kutumia rangi gani? njano
12.Rangi ya njano katika alama za usalama katika
mazingira huwasilishwa kwa kutumika kuwakilisha
alama gani? alama za onyo au tahadhari
13.Alama za usalama katika mazingira za onyo au
tahadhari hutoa maelekezo gani?
i.Kuwa makini
ii.Chukua tahadhari
iii.Hatari katika eneo jirani
14.Rose Alipo kuwa akiendesha gari lake alipoingia
barabara kuu aliongeza umakini zaidi unadhani
alama gani ya usalama ilimwongoza Rose? Alama
ya onyo au tahadhari
15.Alama za usalama wa mazingira za onyo huwa na
sifa gani? zinaumbo la pembe tatu
Picha nyeusi kwenye msingi wa njano na kingo
nyeusi
Andika ndiyo au hapana
16.Alama nyekundu huonyeshwa onyo?__________
17.Alama za kuzuia na kukataza zinakuwa na umbo la
duara na pembe nne?_______
18.Alama za kuzuia au kukataza zinakuwa na mstari
mwekundu?________
19.Rangi ya njano inawakilisha alama za onyo au
tahadhari
20.Kila alama ina umuhimu wake?______
21.Usipo zijua alama za kuchukua tahadhari unaweza
kupata madhara______
Kujibu majibu mafupi
22.Alama za usalama katika mazingiara za amri
hutumia rangi gani? bluu
23.Nini maana ya mazingira? Mazingira ni vitu vyote
vinavyo mzunguka binadamu.
24.Bainisha uhusiano uliopo kati ya mazingira na
uchunguzi wa kisayansi?
Huwezi kufanya uchunguzi wa kisayansi bila
kutumia mazingira
25.Kwanini tunajifunza alama za usalama katika
mazingira? Ili kutusaidia kuepuka na kuchukua
tahadhari ya madhara yatokanayo na vitu
mbalimbali kama moto na ajali mbalimbali
26.Alama za usalama katika mazingiara zinazohusu
amri au lazima hutupa maelekezo gani ? husisitiza
tabia au vitendo Fulani mfano kusisitiza kunawa
mikono
27.Alama za usalama katika mazingira za dharura
hutumia umbo gani? pembe nne (mstatili au
mraba)
28.Alama za usalama katika mazingira zinazotumia
rangi ya bluu huwakilisha alama gani? alama za
lazima au amri
29.Alama za usalama katika mazingira zinazo onesha
dharura hutumia rangi gani kuonyeshwa? Rangi ya
kijani
30.Rangi ya kijani katika alama za za mazingira
hutumika kuwakilisha alama gani? alama za
dharura
31.Alama za dharura za usalama katika mazingira
hutumia rangi gani kuonyeshwa?rangi Kijani
32.Rangi gani katika alama za usalama katika
mazingira hutumika kuonesha madhara makubwa?
rangi nyekundu
33.Bainisha madhara yanayoweza kutokea endapo
hatutafuata alama za tahadhari.

I.Kifo
II.Ulemavu
III.Ajali
IV.magonjwa
34.Orodhesha faida ya kuzijua alama za tahadhari
i.Kuepuka vifo
ii.Kuepuka ajali
iii.Kuepuka magonjwa
35.Chora mchoro kuonesha alama ya tahadhari
katika mazingira inayo onesha hairuhusiwi
kuingia mahali
36.Alama za usalama katika mazingira zinazo kataza
kuingia mahali zina wekwa kwenye maeneo gani?
maabara
37.Bainisha athari za kutokufuata alama ya
kutokuruhusiwa kuingia mahali? Madhara ya kiafya
38.Chora mchoro kuonesha alama inayoelekeza
hairuhusiwi kuvuta sigara
39.Bainisha sehemu ambazo alama ya kutoruhusiwa
kuvuta sigara inachorwa
i.Vituo vya mafuta
ii.Kwenye ndege
iii.Sehemu za mikusanyiko ya watu wengi
iv.Kwenye migahawa
40.Bainisha madhara yanayoweza kutokea endapo
hautofuata alama inayokataza kuvuta sigara eneo
hilo
i.Kusababisha milipuko
ii.Madhara ya kiafya
41.Chora mchoro kuonesha alama inayowakilisha
kutoruhusiwa kunywa wala kula
42.Alama inayowakilisha kutoruhusiwa kula wala
kunywa inachorwa maeneo gani?
Maabara
43.Kutaja madhara yanayoweza kutokana na
kutokufuata alama inayozuia kula wala kunywa?
i.Kifo
ii.Madhara ya kiafya
44.Chora alama inayowakilisha kuonesha vitu vinavyo
vunjika
45.Alama za mazingira inayowakilisha vitu vinavyo
vunjika huchorwa maeneo gani? vyombo vya kioo
au glasi
46.Bainisha madhara yanayoweza kujitokeza endapo
hautafuata alama inayoelekeza kuonyesha vitu
vinavyovunjika? kupata hasara
47.Chora alama ya usalama ya mazingira inayoonesha
maji yasiyo salama
48.Bainisha sehemu ambapo alama ya usalama katika
mazingira ya kuonesha maji yasiyosalama
huchorwa.kwenye mabomba ya maji yasiyofaa kwa
matumizi ya binadamu
49.Bainisha mashara yanayoweza kutokea endapo
hautafuata alama inayoelekeza kuwa maji sehemu
hiyo sio salama.kusababisha madhara ya kiafya
50.Chora mchoro kuonesha alama ya usalama
katikamzaingira inayo onesha vilipuka
51.Alama ya usalama katika mazingira inayo onesha
vilipuaka huchorwa maeneo gani?
i.Sumu za kuua magugu
ii.Dawa za rangi za mafuta
iii.Kemikali zinazotumika maabara
52.Baisha madhara anayoweza kuopata mtu endapo
hatafauata alama inayoonesha vilipuka.kulipuka na
kujeruhi
53.Chora mchoro kuonesha alama inayoonesha
kuchukua tahadhai kitu hicho kinamomonyoa na
kuunguza
54.Bainisha maeneo ambayo alama ya tahadhari
katika mazingiara inayoonesha kuuunguza au
kumomonyoa huchorwa. Kwenye vitu vyenye
kemikali
55.Bainisha madhara yanayoweza kutokea endapo tu
hutafuata alama ya tahadhari inayo onesha
kumomomnyoa au kuunguza .kusababisha
madhara makubwa
56.Chora mchoro kuonesha alama inayoonesha kitu
kinaweza kushika moto.
57.Alama ya usalama katika mazingira inayoonesha
kitu hicho kinaweza kushika moto inachorwa
maeneo gani?
58.Bainisha kemikali zinazochorwa alama ya usalama
katika mazingira ikiwakilisha kuwa kuonesha kitu
hicho kinaweza kushika moto
i.Spiriti
ii.viuatilifu
59.Chora alama ya usalama katika mazingira
inayoonesha kuwa kitu hicho kina kereketa.
60.Alama ya usalama katika mazingira inayoonesha
kuwa kitu hicho kinakereketa huchorwa sehemu
gani.dawa za kuulia wadudu,gundi na rangi za
magari au nyumba.

61.Taja athari zinazoweza kutokea endapo mtu
hatafuata alama ya kuonesha kitu hicho
kinakereketa
Madhara ya kiafya makubwa ya muda mrefu
62.Bainisha madhara yanayoweza kutokea endapo
mtu hatachukua tahadhari inayoonesha kuwa kitu
hicho kinashika moto
Inaweza kusababisha ajali ya moto.
63.Chora mchoro unaoonesha kuwa kitu kinasumu au
ni hatari
64.Alama ya tahadhari inayoonesha kitu kinasumu au
hatari huchorwa maeneo gani
i.Dawa za kuogeshea mifugo
ii.Sumu za kuua wadudu na wanayama
waharibifu
iii.Kwenye transfoma na nguzo za umeme
65.Bainisha madhara yanayoweza kujitokeza endapo
mtu hatazingatia vitu vilivyochorwa kuonesha kitu
hichokina sumu au ni hatari. kifo
66.Chora mchoro kuonesha alama inayoonesha
msongo mkubwa wa umeme
67.Taja mahali ianapochorwa alama inayoonesha
msongo mkubwa wa umeme .sehemu zenye
msongo mkubwa wa umeme.
68.Taja athari zinazoweza kujitokeza endapo mtu
hatachukua tahadhari ya sehemu zilizochorwa
msongo mkubwa wa umeme.kifo
69.Chora mchoro kuonesha alama inayoonesha kuwa
kitu hicho kinaweza kumdhuru binadamu.
70.Chora mchoro wa alama ya usalama kuonesha
mionzi mikali
71. Bainisha sehemu ambapo alama ya usalama ya
mionzi mikali huchorwa. Chumba cha esksirei (x-
ray)
72.Bainisha athari zinazoweza kujitokeza endapo
hautafuata tahadhari kwa alama ya mionzi mikali.
I.Upofu
II.Kuharibika kwa ngozi
III.Saratani
73.Chora mchoro kuonesha alama ya usalama
inyoonesha uwepo wa vimelea vya magonjwa.
74.Mchoro wa alama ya usalama kuonesha uwepo wa
vimelea vya magonjwa huchorwa sehemu gani?
I.Vyombo vya kuhifadhia sampuli
II.Vifaa vya kutupia mbabaki ya sampuli
75.Bainisha madhara yanayoweza kujitokeza endapo
mtu hatafuata na kuchukua tahadhari kwa vitu
vilivyochorwa mchoro wa usalama kuonesha
uwepo wa vimelea vya magonjwa
I.Huweza kupata maambukizi ya magonjwa
76.Chora mchoro wa usalama kuonesha kuchukua
tahadhari ya uteleze katika sakafu
77.Alama ya usalama katika mazingira kuonesha
uwepo wa utelezi huchorwa maeneo gani?
I.Sehemu inayoteleza
II.Kwenye maji
78.Orodhesha madhara yanayoweza kutokea endapo
mtu hatafuata tahadhari ya kuonesha kuna utelezi.
I.Kuanguka
II.Kuumia
III.kuteleza
79.Chora mchoro wa alama za usalama katika
mazingira kuonesha hatari
80.Alama ya usalama katika mazingira kuonesha
hatari inachorwa maeneo gani?
I.Sehemu yenye matengenezo ya barabara
81.Bainisha madhara yanayoweza kutokea endapo
mtu ahatafuata uwepo wa alama ya tahadhari
kataika mazingira inayoonesha uwepo wa hatari
I.Ajali na kusababisha vifo
82.Chora mchoro wa alama za usalama katika
mazingira unao onesha kuelekeza unaaji mikono.
83.Bainisha athari zinazoweza kujitokeza endapo mtu
hatafuata tahari ya alama ya usalama katika
mazingira inayoonesha kunawa mikono.
I.Kupata maambukizi ya magonjwa
84.Chora mchoro wa alama ya usalama kuonesha
kujikinga macho
85.Taja sehemu inapochorwa alama ya usalama katika
mazingira inayoonesha kujikinga macho.
Sehemu zenye mionzi
86.Taja madhara yanayoweza kutokea endapo mtu
hatafuata alama ya mazingira inayoonesha
kujikinga macho.athari za macho
87.Chora mchoro wa alama ya usalama katika
mazingira kuonesha njia au mlango wa kutokea
wakati wa hatari
88.Taja sehemu inapochorwa alama ya usalama katika
mazingira inayoonesha sehemu au mlango wa
kutokea inapotokea hatari.majengo ya hospitali
89.Bainisha madhara yayoweza kutokea endapo mtu
hatafuata alama ya usalama katika mazingira
inayoonesha sehemu au mlango wa kutokea
wakati wa hatari huweza kupata ajali na kupekea
kifo
90.Nini maana ya usalama katika mazingira?ni alama
ambazo hutoa taarifa kuhusu hatari iliyopo kwenye
vitu au mazingira,na alama hizo hutoa maelekezo

ambayo hupelekea kulinda usalama wa vitu na
viumbe hai katika mazingira.
91.Bainisha tofauti iliyopo kati ya alama ya usalama
inayoonesha mlango wa kutokea na ile inao
onesha uwepo wa utelezi
Maumbo
Mlango wa kutokea
utelezi
Rangi
Mlango wa kutokea
utelezi
Mkao wa watu walioko katika alama hizo
Mlango wa kutokea________________________
Uteleza__________________________________
92. Bainisha tofauti kati ya alama ya mazingira
inayowakilisha kujikinga macho na ile ya kujikinga.
93.Orodhesha ufanano uliopo kati ya alama za
usalama katika mazingira inayohusu maji
yasiyosalama na ile ya kuelekeza uoshaji mikono
94.Orodhesha alama za usalama katika mazingira
zinazochorwa kwa ktumia alama ya pembe tatu
95.Taja alama za usalama katika mazingira
zinazochorwa kwa kutumia mchoro wa duara
96.Taja alama za usalama katika mazingira
zinazochorwa kwa kutumia mchoro wa pembe nne
97.Ainisha alama za usalama katika mazingira ambazo
zinatumia mfano wa mtu katika kutoa tahadhari
98.Bainisha tofauti iliyoo kati ya alama ya usalama
katika mazingira ya kutoa tahadhari ya utelezi na
ile ya kuonesha sehemu hiyo haruhusiwi kuingia
99.Orodhesha alama za usalama katika mazingira
zinazoonesha uwepo wa hatari
100.Bainisha matumizi ya alama za usalama katika
mazingira
101.Taja alama za usalama katika mazingira zinazo
onesha kutuepusha na magonjwa
102.Bainisha alama za usalama katika mazingira
zinazotusaidia na kutuepusha na ajali
103.Orodhesha alama za usalama katika mazingira
zinazo toa tahadhari
MADA YA SHATI YA UMEME
1.Nishati nini?
2.Taja vyanzo vya nishati a…….b……..c……d……e……f……
g……
3.Kwanini nishati ya umeme huitwa nishati kibebeo
4.Kupwa na kujaa kwa maji kunatokana na nini?
5.Taja njia za kuzalisha umeme
6.Mawimbi katika bahari hutokana nanini?
7.Kupwa na kujaa kwa maji nini?
8.Mkondo wa maji unaosababishwa na kupwa na kujaa
kwa maji unaweza kutumika kuzalisha nini?
9.Mtambo unaozalisha umeme kwa kutumia mkondo
wa maji hufanana na mtambo gani?
10.Taja faida ya kuzalisha umeme kwa kutumia
mawimbi na mkondo wa maji?
11.Taja hasara za kuzalisha umeme kwa kutumia
mawimbi na mkondo wa maji
Andika ndio au hapana
12.Tunaweza kuzalisha umeme kwa kutumia mawimbi
ya maji
13.Kupwa na kujaa kwa maji ni chanzo cha umeme
14.Nishati ya umeme huzalishwa kwa kutumia mafuta
na gesi tu
15.Mvutano kati ya dunia na mwezi ni chanzo cha
umeme
16.Umeme unazlishwa na mkondo wa umeme
haupatikani wote
17.Umeme hutokana na mawimbi ya mkondo wa
umeme ni rafiki kwa mazingira
18.Viumbe hai wanaweza kuathiriwa na mtambo wa
kuzalisha umeme
19.Chora mchoro kuonesha a]mtambo wa kuzalisha
umeme kutokana na mawimbi ya bahari[b]kuzalisha
umeme kwa ktumia mkondo wa umeme
20.Magma hupatikana wapi?
21.Magma hupatikana ardhini kupitia kwenye nini?
22.Maji na miamba iliyo karibu na magma huweza
kuathiri kwa njia gani?
23.Uzalishaji wa umeme kwa kutumia joto ridi hutumia
zaid?
24.Jotoridi linaweza kuzalishwa umeme kwa kutumia
nini?
25.Mtambo wa kuzalisha umeme umeundwa na
……….inayozungushwa kwa mvuke
26.Mvuke wa kuzalisha umeme kwa kutumia joto ridi
huvutwa kwa ………kwenye mtambo ardhini
27.Mvukke unatumika kuendesha tabaini hupoa na
kurejeshwa ardhini kwa kutumia nini?
28.Taja faida za kuzalisha umeme kwa kutumia joto ridi
a]……..b]
29.Kuainisha hasara za kuzalisha umeme kwa kutumia
jotoridi
30.Bainisha ubora wa nishati ya jadidifu ………
31.Taja athari za kutumioa nishati jadidifu……………
32.Vyanzo vya nishati jadidifu ni kama vile nini
33.Vyanzo vya umeme vinavyotokana na maji nini?

34.Mtambo wakuzalisha umeme ambao hautumii
tanabaini ni mtambo gani
Andika ndio hapana
35.Nishati ya umeme huzalishwa kwa kutumia mafuta
ya gesi vunde tu?
36.Rasmali za kuzalisha nishati jadidifu zinatokana na
michakato ya asili
37.Mawimbi ya maji maporomoko ya maji na jotoridi ni
baadhi ya vyanzo vya uzalishaji wa umeme
38.Gharama za kutengeneza na kufunga mitambo ya
kuzalisha nishati ya umeme jadidifu ni ndogo?
39.Nishati ya umeme itokanayo na upepo inategemea
uwepo wa upepo wenye kasi kubwa
40.Orodhesha faida mbili za nishati jadidifu
41.Kwa kutumia mifano tofautisha kati ya nishati
jadidifu na nishati isiyojadidifu
42.Tofautisha ufuaji wa nishati ya umeme kutokana na
jua na ule wa jotoridi?
43.Kwanini nishati jadidifu huitwa nishati endelevu
44.Chanzo kipi nirahisi kutumika katika uzalishaji wa
umeme kulingana na mazingira?........na kwanini
45.Bainisha faida ya nishati ya umeme unaotokana na
mawimbi ya bahari
46.Kwanini baadhi ya vitu huzama na vingine havizami?
47.Andika kanunu ya kutafuta density
48.Kizio cha tungamo nini?
49.Kizio cha density nini?
50.Kizio cha ujazo nini?
51.Tafuta density ya kitu chenye tungamo ya 500 na
ujazo wa sentimeta 50
52.Kwanini kipande cha chuma kikiwekwa kwenye maji
pamoja na kipande cha mbao kipande cha chuma
kinazama?
53.Kipi kati kitu chenye density kubwa na kile che
density ndogo [a] kitaelea kwenye maji [b]kitazama
kwenye maji
54.Nini maana ya density?
55.Tafuta density ya kitu chenye tungamo ya kg 2000 na
ujazo wa meta 1000
56.Nini kitatokea endapo density ya kitu itakuwa kubwa
kuliko density ya maji?
57.Nini kitatokea pale density ya kitu itakuwa ndogo
kuliko density ya maji?
58.Tafuta density ya kitu chenye tungamo ya kg 600 na
ujazo wa sentimeta 100?
59.Orodhesha mambo yanasababisha vitu vizame au
kuelea kwenye maji
60.Kwa kawaida kitu chenye uwazi kinaweza kulea au
kuzama?
61.Kwanini kitu chenye uwazi ndani hakizami kwenye
maji?
62.Kutaja mfano wa vitu vinavyoelea kwenye maji
ambavyo vina uwazi ndani
63.Nini kitatokea iwapo kani elezi ikiwa ndogo kulikao
kani mvauatanno?
64.Kwanini sarafu huzama kwenye maji?
65.Vitu vinavyo zama au kuelea kwenye maji huathiriwa
na nini?
66.Kani elezi ni kani ambayo husukuma vitu kuelekea
wapi?
67.Kani uvutano ni kani inayovuta vitu kuelekea wapi?
68.Kizio cha kani ya uvutano nini?
69.Kizio cha kani uvutano huwakilishwa kwa herufi
gani?
70.Kani uvutano hupimwa kwa kutumia kipimo gani?
71.Chora mchoro kuonesha kipimo cha mizani ya springi
72.Kani ya uvutano ni zao la nini?
73.Kizio cha mchapuko wa uvutano nini?
74.Tungamo nini?
75.Kani ya mvutano au uzitohuwakilishwa kwa kutumia
harufi gani?
76.Kizio cha uzito nini?
77.Andika kanuni ya kutafuta uzito wa kitu
78.Tafuta uzito wa kitu chenye tungamo kg 2000 wa
mchepuko wa uvutano meta kwa sendunde 50
79.Kama kani ya uvutano ni ndogo kuliko kani elezi nini
kitatokea?
80.Nini maana ya density?
81.Kanini meli inaelea lakini sindano inazama?
82.Taja sifa mbili za vitu vinavyoelea kwenye maji
83.Taja matokeo yake baada ya kwekwa kwenye maji
Kitu matokeo yake
A.jani
B.msumari
C.ufutio
D.kichongeo
E.kijiko cha chuma
F.kijiko cha plastiki
G.jiwe
H.penseli
I.sindano
J.meli
K.unyoya
L.ndoo
M.karatasi
N.sahani ya bati

O.kikombe cha udongo
P.sufuria
Q.jahazi
R.ubao wa mbao
84.mwanayansi archimedesi anatoka nchi gani?
85.Mwanasayansi archimedesi aliishi kuaniz mwaka
gani?...hadi lini….
86.Taja kanunu ya archimedesi……………………………….
87.Bainisha mambo mawili anayo yatumia
mwanasayansi Archimedes kuthibitisha kanunu yake
a……………………………………………..b…………………………..
88.Kwa mujibu wa kanuni ya mwanasayansi archimedesi
kitu kikiwa kwenye maji kinaitwa je?
89.Kwa mujibu wa kanuni ya archimedesi kitu kikiwa nje
ya maji kinaitwa je?
90.Jiwe lina uzito wa newton 400 likiwa hewani,likiwa
limezama kwenye ugiligili uzito wake ni newton
50.tafuta kanielezi inayosukuma jiwe hilo
91.Ukumbwa wa kani elezi nini?
92.Kitu kinachoelea wakati kimezama kituhicho
kimeathiriwa nanini?
93.Ili kitu kielee lazima kani elezi na kani uvutano ziwe
katika hali gani?
94.Taja kanuni ya kani elezikwa kitu
95.Taja matumizi mawili ya kanuni ya kuelea kwa vitu
96.Kwanini meli haizami kwenye maji?
97.Kwanini nyambizi huzama na kuelea kwenye maji?
98.Nini hufanya kitu kuelea na kuzama kwenye maji?
99.Kama desnsity ya kitu ni ndogo kuliko desnsity ya
maji nini kinatokea?
100.Nyambazi huzama kwenye maji pale density yake
ikiwa katika hali gani?
101.Taja sababu ya vitu kuelea na kuzama kwenye maji
102.Kuna uhusiano gani kati ya uzito wa kitu
kinachoelea kwenye ugiligili wa kanielezi
103.Elezea kanuni ya kuelea inayotumika kuunda meli?
104.Kuna uhusiano gani kati ya uzito wa umbo unaoelea
kwenye maji na uzito wa maji yaliyohama wakati
ubao umeingizwa kwenye maji?
105.Tafuta density ya kitu chenye tungamo ya kg240 na
ujazo wa meta 40
106.Density ya kitu ni kg 160 kwa meta moja ya ujazo
ikiwa tungamo ni kg 280 tafuta ujazo wake?
107.Elezea maana ya kani elezi?
108.Nini maana ya kani uvutano?
109.Nyambizi nini?
110.Tungamo nini?
111.Ugiligili nini?
1.Antenna nini
2.Kifaa kinachotumika kunasa na kusambaza mawimbi
sumaku umeme kwenye vifaa vya mawasiliano kama
vile redio,simu za mkononi na runinga huitwa?
3.Taja vifaa sita vianvyotumia antenna
4.Upokeji na usambazaji wa mawimbi hufanywa na
kifaa gani ?
5.Hatua ya kwanza katika usambazaji wa mawimbi ya
sauti kutoka katika mtangazaji wa redio ni ipi?
6.Mtangazji wa redio anapatoa matangazo kwa njia ya
sauti mawimbi ya sauti hubadilishwa na kuwa
7.Baada ya mawimbi ya sauti kubadilishwa kuwa
mawimbi umeme husafirishwa kwneda kwenye
nini?
8.Kuaja kazi mbili ya antenna iliyofungwa kwenye
kituo cha matangazo?
9.Baadhi ya mawimbi husafirishwa kwenye antenna
iliyofungwa kituyo cha matangazo nini kinatokea
10.Mawimbi yanayopokelewa na antenna redio
hubadilishwa na kuwa mawimbi gani
11.Antena ya redio hubadilisha mawimbi sumaku kuwa
mawimbi
12.Taja vyombo kumi vya usafiri vinavyotumia antenna
13.Sakiti ya umeme iliyounganishwa na redio hubadili
mawimbi sumaku umeme kuwa mawimbi gani?
14.Rada nini?
15.Taja kazi za roda a]………………
b………………………….c………………….
16.Taja aina mbili za antenna ambazo zinaweza kupokea
na kusambaza mawimbi
17.Orodhesha antenna ambazo zinaweza kupokea
mawimbi tu
18.Bainisha umuhimu wa antenna
19.Somo la antenna linakusaidia nini kama
mwanafunzi?
20.Kuna aina ngapi za antenna?
21.Taja aina tano za antenna
22.Antena waya kwa kiasi kikubwa imeundwa na nini?
23.Taja sifa tatu za antenna waya
24.Taja aina tatu antenna waya
25.Antena kitanzi hupatikana katika maumbo gani?
26.Chora mchoro kuonesha maumbo ya antena kitanzi
27.Taja matumizi ya antena kitanzi
28.Ainisha faida 6 za kutumia antena kitanzi
29.Taja hasara tatu za kutumi antena kitanzi
30.Antena kipenyo hujumuisha antena kama vile
31.….ni antena yenye umbo la bomba lenye uwazi
mpana upande mmoja na uwazi finyu kweny kitako
32.Antena mpenyo huwa na sifa gani?

33.Taja sifa tatu za antena honi
34.Antena honi hutumika kwenye nini?
35.Taja faida za antena honi?
36.Bainisha hasara za kutumia antena honi?
37.Chora mchoro kuonesha anatena honi
38.Nini maana ya antena safu?
39.Antena safu hujumuisha antena gani?
40.Mgunduzi wa antena yagi-uda anatoka nchi gani?
41.Antena yagi-uda ilitokana na nini?
42.Bainisha vifaa 5 vinavyounda antena yagi-uda
43.Taja namna yagi-uda ambavyohufanya kazi
44.Chora mchoro kuonesha antena ya yagi-uda
45.Taja faida 5 za kutumia antena ya yagi-uda
46.Bainisha hasara tatu za kutumia antena ya yagi-uda
47.Tofautisha kati ya antena ya yang-uda na antena akisi
48.Bainisha muundo wa antena akisi
49.Antena akisi huwa inafananishwa na kitugani?
50.Taja kazi ya antena akisi
51.Taja vifaa vinavyounda antena akisi
52.Taja mfano wa antena akisi
53.Antena mchirizo akisi au dishi nini?
54.Kwanini antena mchirizo hujulikna kama antena ya
sahani?
55.Ubora wa antena mchirizo hutegemea nini?
56.Taja kazi ya antena mchirizo
57.Taja vifaa 4 vinavyounda antena mchirizo
58.Taja faida 3 za kutumia antena mchirizo
59.Taja hasara 4 za kutumia antena mchirizo
60.Chora mchoro kuonesha sehemu za antena mchirizo
61.……………ni aina ya antena ambayo ni nyepesi na
yenye umbo bapa
62.Taja vifaa viwili vinavyounda antena kidoa
63.Antena kidoa imeundwa na metali ngapi?
64.Taja metali 2 zinazounda antena kidoa
65.Metali bapa ndogo kwenye antena kidoa huwakilisha
upande gani?
66.Metali bapa kubwa kwenye antena kidoa huwakilisha
upande gani?
67.Chora mchoro kuonesha antena kidoa
68.Uwezo wa kupokea na kuchakata mawimbi kwenye
antena kidoa hutegemea kitu gani?
69.Nini matokeo kati ya umbali kuwa mkubwa kati ya
metali bapa kubwa na metali bapa ndogo ?
70.Nini matokeo kati ya umbali kuwa mdogo kati ya
metali bapa kuwa mkubwa?
71.Taja vifaa 4 ambavyo hutumiwa na antena kidoa
72.Chora mchoro kuonesha antena kidoa
73.Taja faida 4 za kutumia antena kidoa
74.Bainisha hasara 3 za kutumia antena kidoa
75.Ili antena kidoa iweze kufanya kazi vizuri inatakiwa
iwe na sifa gani?
76.Taja namna antena mchirizi akisi umbo lake linavyo
isaidia kuwa na ubora
77.Taja sifa 4 za antena chirizo akisi
78.Taja antena 3 ambazo zinakuwa na ubora kulingana
na maumbo yake
79.Bainisha sifa zinazoweza kusaidia antena waya kuwa
bora na kufanya kazi kwa ufanisi
80.Bainisha sifa 4 ambazo husaidai antena kuwa bora
81.Kizio cha kupima masafa ya usafirishaji wa mawimbi
ya sauti ni?
82.Antena honi na antena yagi-uda zinaweza kusambaza
mawimbi ya masafa marefu katika vipimo gani?
83.Giga hezi moja ni sawa na Hezi ngapi?
84.Giga Hezi [GHZ] ni kipimo cha kupimia nini?
85.Hezi bilioni moja ni sawa na GHZ ngapi
86.Taja ufanisi wa antena zifuatazo katika kusambaza
mawimbi
a.antena honi………………………………
b.yagi-uda……………………………………..
c.Antena kitanzi……………………………………….
87.Kwanini antena Yagi-uda inaufanisi zaidi katika
kupokea mawimbi?
88.Antena Yagi-uda hupokea mawimbi kuwa masafa
marefu katika megehezi ngapi?.......hadi ngapi…..
89.Taja antena zinazotumika katika masafa marefu au
mafupi kupokea mawimbi nini?
90.Ni kwanamna gani ufanisi wa antena unachagia
ubora wa antena ?
91.Kwanini antena honi inafanya kazi kwa ufanisi zaidi?
92.Ufanisi wa antena kupokea mawimbi unaweza
kuboreshwa kwa njia gani?
93.Antena honi na mchirizo akisi hutumika katika vifaa
gani?
94.Taja hatua tano za kutengeneza antena
95.Antena haiwezi kutengenezwa kwa ajili ya matumizi
gani?
96.Bainisha mambo matatu yanayohitajika kufanyika
wakati wa kusanifu antena
97.Yag-uda ina sehemu kuu ngapi?
98.Taja sehemu 2 za antena ya Yagi-uda
99.Kuna aina ngapi za element katika antena Yagi-uda
100.Taja elementi 3 zinazounda antena Yagi-uda
101.Elementi kiakisi hupatikana wapi kwenye antena ya
Yagi-uda?
102.………………nisehemu amabapo mawimbi ya
nakutana na kitumi

103.Elementi ongoza huwa sehemu gani katika antena
Yagi-uda?
104.Taja kazi za kitumi kwenye antena ya Yagi-uda
105.Bainisha kazi ya elementi ongozaji kiakisi na
elementi endeshwaji
106.Nini kazi ya mkonga wa antena kwenye antena
YAGI-UDA?
107.Hatua ya nne katika kutengeneza antena nini?
108.Taja sifa 2 inayoweza kukuongoza wakati wa
kuchagua vifaa vya kutengenezea antena/
109.Taja sababu kwa kila kifaa kimoja Kwanini antena
hutengenezwa kwa vifaa kama vile
A.Shaba………………………..
B.Metali……………………………
C.Aluminium…………………………
D.Chuma cha pua…………………………..
110.Taja hatua ya mwisho kabisa katika kutengeneza
antena
111.Bainisha matumizi matano ya antena
112.Antena zinazotumika kwenye magari huundwa kwa
kutumia vifaa gani?
113.Niana gani ya antena inatumika kwa ajili tu ya simu
za mkononi?
114.Orodhesha antena 2 zinaweza kutumika katika
runinga
115.Katika kunasa mawimbi ya utabiri wa hali ya hewa
antena ipi ni bora zaidi kutumika?
116.Antena gani inauwezo wa kujikinga na kelele kwa
ufanisi
117.Antena kidoa hutumika sana kwenye vifaa gani?
118.Malighafi gani husaidia kuipa antena ufanisi
kwasababu ya uwezo wake wakupitisha umeme?
Mashine tata vii
1.Bainisha tofauti kati ya mashine tata na mashine
rahisi
2.Nini maana ya mashine tata?
3.Taja mfano wa mashine rahisi 5 unazozijua
4.Ainisha mfano wa mashine tata 5 unazozijua
5.Bainisha sehemu 6 zinazounda kitasa
6.Taja kazi za sehemu zifuatazo za kitasa
A.Komeo………………………………………………………
B.Bolti…………………………………………………………
C.Ufunguo……………………………………………………
D.Nyenzo………………………………………………………
E.Springi………………………………………………………..
F.Bolti ya kuingiza mkono………………………………
7.Katika orodha ifuatayo bainisha kama ni mshine
rahisi au mashine tata
A.Toroli……………………..
B.kitasa……………………..
C.Ngazi……………………..
D.Cherehani……………………..
E.baiskeli……………………..
F.Mkasi……………………..
G.Nyundo……………………..
H.Kisu……………………..
I.Mashine ya kusaga……………………..
J.Brenda……………………..
K.Msumari……………………..
L.Bolti……………………..
M.Springi……………………..
N.Ufunguo……………………..
O.Kalamu……………………..
P.Bembea……………………..
8.Taja hatua 4 za kutunza kitasa
9.Bainisha kazi za cherehani
10.Kwanini cherehani ni mashine tata?
11.Kuna aina ngapi za cherehani?
12.Taja sehemu tano zinazounda cherehani
13.Taja kazi za sehemu zifuatazo za cherehani
A.Grudumu la mikono…………………………………..
B.Eskeli…………………………………..
C.Mkanda…………………………………..
D.Gurudumu mtaiombo…………………………………..
E.pedeli…………………………………..
14.bainisha hatua 5 namna ya kutunza cherehani
15.baiskeli ni aina gani ya mashine
16.taja kazi 3 za baiskeli
17.kwanini baiskeli ipo kundi la mashine tata
18.taja sehemu 3 zinazo unda baiskeli
19.kuna aina ngapi za baiskeli?
20.Taja sehemu zinazounda gurudumu kwenye baiskeli
21.Roda katika baiskeli huundwa kwa kutumia vitu gani?
22.Nyenzo katika baiskeli imeundwa kwa kutumia vitu
gani?
23.Chora mchoro kuonesha sehemu za baiskeli
24.Taja hatua tatu namna ambavyo baiskeli hufanya
kazi
25.Taja kazi ya pedeli kwenye basikeli
26.Taja kazi ya gurudumu kwenye basikeli
27.Bainisha matokeo ya pedeli inapojizungusha
28.Bainisha kazi ya mnyororo kwenye basikeli
29.Nini matokeo ya gurudumu la nyuma la baiskeli
kuzungushwa na mnyororo
30.Bainisha namna ya kutunza baiskeli
31.Taja sehemu ambapo kwenye baiskeli huwekwa
vilainishi

32.Kwanini tunashauriwa kutumia vilainishi kwenye
baiskeli
33.Taja kazi atau za mashine ya kusaga
34.Mashine ya kusaga ni ana gani ya
msahine………………………….na kwasababu gani?
35.Taja sehemu 7 zinazounda mashine ya kusaga
36.Mashine ya kusaga ina mshine sahili ngapi?
37.Taja msahine sahili tatu zinazounda mashine ya
kusaga
38.Gurudumu ekseli huzungushwa na nini?
39.Taja vitu vinavyounda roda katika mshine ya kusaga
40.Mashine inaweza kuendeshwa kwa kwa kutumia
nishati gani?
41.Taja namna mashine inayoendeshwa kwa kutumia
injini inavyofanya kazi
42.Mashine inayotumia injini ya fueli hubadili nishati ya
fueli kuwa nishati ya
43.Mashine inayotumia mota ya umeme hubadili nishati
……..kuwa nishati ya……..
44.Kuchora mchoro kuonesha sehemu za mashine
yakusaga
45.Bainisha hatua 5 za namna ya kutunza mashine ya
kusaga
46.Taja kazi ya sehemu zifuatazo kwenye mashine
A.Bomba…………………………………..
B.Kitambaa…………………………………..
C.Mteremko…………………………………..
D.Ekseli…………………………………..
E.Gurudumu dogo…………………………………..
F.Mkanda…………………………………..
G.Durudumu kubwa…………………………………..
H.Ekseli kubwa…………………………………..
47.Bapa nisehemu ya mashine gani?
48.Mota katika blenda hubadilisha nishati ya umeme
kuwa nishati ya
49.Nishati katika mashine ya kusaga husafirishwa
kutoka kwenye mota hadi kwenye kinu kwa kutumia
nini?
50.Sehemu ya kutumbukiza ufunguo katika kitasa ina
mshine sahili aina ya
51.Cherhani hulainishwa kwa kutumia nini?
52.Ili cherehani idumu kwa muda mrefu ni muhimu
kufanya mambo gani?
53.Blenda nini?
54.Mashine ndogo inayotumika kutengeneza juisi
huitwa?
55.Taja kazi 3 ambazo blenda inaweza kufanya
56.Kwanini blenda huwekwa katika kundi la mshine tata
57.Taja muundo wa mashine ya blenda
58.Mota ya blenda inapatikana kwenye nini?
59.Mota hubadilisha nishati ya umeme kuwa nishati
gani?
60.Chora mchoro kuonesha blenda
61.Ainisha namna blenda inavyofanya kazi
62.Kutaja klazi ya sehemu zifuatazo za blenda]
A.Blenda…………………………………..
B.Mota…………………………………..
C.Ekseli…………………………………..
D.Bapa…………………………………..
63.Bainisha namna ya kutunza blenda
Moto
1.Moto nini?
2.Ili moto uwake unahitaji vitu gani?
3.Gesi gani inasaidia mota uwake?
4.Fueli nini?
5.Taja hali ambazo Fueli inaweza kuwa ?
6.Chora mchoro kuonesha mchoro wa moto katika
umbo la pembe tatu
7.Taja fueli ya vyanzo vya moto vifuatavyo
A.Moto wa kuni…………………………………..
B.Moto wa gesi…………………………………..
C.Moto wa mafuta …………………………………..
D.Jiko la mafuta ya taa…………………………………..
E.Kibatari…………………………………..
8.Orodhesha umuhimu 6 wa moto katika maisha ya
kila siku
9.Bainisha sababu 10 zinazoweza kusababisha ajali ya
moto
10.Taja madaraja 5 ya moto
11.Bainisha vyanzo vya moto kulingana na maraja
yafuatayo
A.Moto daraja la A…………………………………..
B.Moto daraja la B…………………………………..
C.Moto daraja la C…………………………………..
D.Moto daraja la D…………………………………..
E.Moto daraja la F…………………………………..
12.Bainisha vifaa vinavyotumika kuzima moto katika
madaraja yafuatayo
A.Moto daraja la A…………………………………..
B.Moto daraja la B…………………………………..
C.Moto daraja la C…………………………………..
D.Moto daraja la D…………………………………..
E.Moto daraja la F…………………………………..
13.Taja madaraja ya moto ambayo huweza kuzimwa
kwa kutumia maji
14.Moto wa daraja A hutokana na vitu vyenye asili ya
yabisi kama vile vitu gani?
15.Taja vitu 4 vinavyotumika kuzima moto daraja A

16.Moto daraja B hutokana na vyanzo gani?
17.Taja vyanzo 5 vya moto daraja B
18.Moto katika daraja B katika hatua za awali huweza
kuzimwa kwa kutumia vitu gani?
19.Taja vifaa vinavyotumika kuzima moto daraja B
20.Orodhesha madaraja 3 ambayo moto wake huweza
kuzimwa kwa kutumia hewa au gesi ya
kabonidayoksidi
21. Taja gesi inayopatikana kwenye mitungi yenye rangi
ya
A.Rangi nyeusi…………………………………..
B.Rangi ya bluu…………………………………..
22.Moto daraja D ni moto unaotokana nani? Taja vynzo
hivyo
23.Taja vitu vinavyo tumika kuzima moto wa daraja la
C?
24.Taja vyanzo vya moto daraja D
25.Bainisha vitu vinavyo tumika kuzima moto daraja D
26.Taja chanzo cha moto daraja D
27.Moto katika daraja F huzimwa kwa kutumia nini?
28.Moto unaosababishwa na umeme hauwezi kuzimwa
kwa kutumia nini?
29.Kwanini hatuwezi kuzima moto unaosababishwa na
umeme kwa kutumia maji?
30.Taja vifaa vinavyo tumika kuzima moto
unaosababishwa na umeme
31.Kabla ya kuzima moto unao sababishwa na umeme
hatua ya kwanza unatakiwa kufanya nini?
32.Kwanini tunashauriwa kutumia mchanga
mkavu ,poda kavu na kabonidayoksidi kuzima
umeme unaosababishwa na umeme badala ya
kutumia maji?
33.Taja hatua 4 za kuzima moto
34.Taja vifaa vinavyotumika katika hatua za awali za
kuzima moto
35.Moto ukiwa mkubwa kinanani wanahusika kuzima
moto huo?
36.Orodhesha mambo yanayotakiwa kuzingatiwa wakati
wa kuzima moto
Tindikali na nyongo
1....………….. ni dutu ya ya kemikali ambayo ina ladha ya
uchachu
2.Dutu nini?
3.………………ni vitu vilivyopo katika hali iliyosawa.
4.Taja vyakula 4 vyenye tindikali
5.Kuna aina ngapi za tindikali?
6.Taja aina 4 za tindikali za asili
7.Taja aina 2 za tindikali
8.Asetiki ni aina gani ya tindikali?
9.Laktiki ini aina gani ya tindikali?
10.Tindikali ya asetiki hupatikana kwenye nini?
11.Tindikali ya lakitiki za asili hupatikana kwenye nini?
12.Tindikali gani inapatikana kwenye mfumo wa chakula
wa myama?
13.Tindikali ya asil;I ya haidrokloriki hupatikana wapi?
14.Taja kazi ya tindikali za asili
15.Ainisha tindikali 2 ambazo sio za asili
16.Tindikali sizizo za asili hutengenezwa wapi?
17.Taja matumizi 6 za tindikali zisizo za asili
18.Bainisha matumizi ya tindikali
19.…..ni dutu la kemikali ambayo ina ladha ya uchungu
na inateleza
20.Bainisha sehemu 3 ambazo tunaweza kupata
nyongo
21.Taja matumizi 4 ya ngongo
22.Ainisha viashiria vya uwepo wa nyongo
23.Kutu nini?
24.Kutu hutokana na nini?
25.Taja vitu vinavyoweza kuwa na kutu
26.Takataka nini?
27.Taja vyanzo vya takataka
28.Takataka zinaweza kugawanywa katika mafungu
mangapi?
29.Taja makundi matatu ya takataka
30.Orodhesha njia tatu za kuteketeza taka
31.Bainisha maumizi 4 mazuri ya takataka
32.Taja faida 10 za kuteketeza takataka
33.Taja hatua 3 za kuteketeza takataka
34.Kwanini zoezi la uteketezaji taka huzingatia utaratibu
maalum?
35.Bainisha makundi 6 ya takataka
36.Tajaaina 4 za takataka zinazoteketezwa kwa moto
37.Katika vipengele vifuatavyo bainisha aina za taka
katika kila kundi
A.Taka
zisizoungua………………………………………………
B.Taka
hatarishi……………………………………………………
C.Taka zisizo
hatarishi……………………………………………………
D.Taka zenye atahari wakati wa
kuteketeza…………………………………………………
E.Taka zisizo na athari wakati wa
kuziteketeza………………………………………………
38.Katika makundi ya fuatayo kwa kila kundi bainisha
aina ya taka inayopatikana katika hilo kundi
A.Chombo cha rangi ya
bluu…………………………………………………………

B.Chombo cha rangi ya
njano…………………………………………………………
C.Chomvbo cha rangi ya
kijani…………………………………………………………
D.Chombo cha rangi
nyekundu…………………………………………………
E.Vhombo cha rangi ya
kijivu…………………………………………………………
F.Chombo cha rangi ya
chungwa……………………………………………………
39.Kwanini tunashauriwa kuchagua eneo sahihi la
kuteketeza takataka?
40.Taja njia 4 za kuteketeza takataka
41.Mambo gani 3 ya kuzingatia unapochagua njia ya
kuteketeza taka
42.Njia ya kuzipondaponda takataka hutumika
kuteketeza taka za aina gani?
43.Taja mfano wa takataka 4 zinazoteketezwa kwa njia
ya kuzivunjavunja
44.Njia ya kuchoma moto takataka hutumika kuteketeza
takataka zenyesifa gani?
45.Taja faida 3 ya kuteketeza taka kwa njia ya moto
46.Taja athari 4 zinazotokana na kuteketeza taka kwa
njia ya moto
47.Njia ya kuteketeza takataka kwa kutumia kemikali
hutumika kwenye takataka zenye sifa gani
48.Orodhesha aina 3 za taka zenye kemikali
49.Mambo gani ya kuzingatia wakati wa kuteketeza
takataka zenye kemikali
50.Uteketezaji wa taka kwa njia ya tanuru hutumika
kuteketeza taka zenye sifa gani?
51.Orodhesha mfano wa taka zinazoteketezwa kwa njia
ya tanuru
52.Tanuru nini
53.Taja sifa za mahali panapofaa kujenga tanuru la
kutekezea taka
54.Taja sehemu 3 ambapo hutumia tanuru kuteketeza
takataka
55.Taja sehemu zinazounda tanuru la kuchomea
takataka
A.Bainisha kazi za sehemu zifuatazo za tanuru
la kuchomea takataka Sehemu ya kuingizia
hewa na kutolea
hewa…………………………………………………………
B.Dohari……………………………………………………….
Mlo kamili
1.Mlo kamilinini?
2.……ni vitu vinavyochangia mwili kuwa katika afya
bora
3.Mlo kamili nini?
4.……..ni uwiano sahihi wa makundi ya vyakula
5.Taja makundi matano ya vyakula yanayo wakilisha
mlo kamili
6.Taja aina 6 ya vyakula kutoka kundi la vyakula vya
protini
7.Kazi ya vyakula vya protini katika mwili nini? taja kazi
mbili
8.Taja makundi 6 ya vyakula kutoka kundi la vyakula
vya protini
9.Taja kazi kuu 2 za vyakula kundi la kabohaidreti
10.Mtu anayefanya kazi ngumu anashauriwa kula
vyakula gani?
11.Mtu anayeku;a vyakula vya kabohaidreti kwa wingi
anaweza kufanya shughuli gani?
12.Taja aina 4 za vyakula aina ya mafuta
13.Kazi kuu ya vyakula vyenye mafuta mwilini nini? taja
kazi mbili
14.Taja aina 8 ya vyakula vinavyo upa mwili vitamin
15.Bainisha kazi ya vyakula vyenye vitamin mwilini
16.Chakula gani hufanya kazi kama sseli nyeupe za
damu?
17.Taja magonjwa ambayo huweza kuzuiwa kwa kula
mlo kamili
18.Kwanini tunashuriwa kunywa maji ya kutosha?
19.Taja kazi 5 za maji mwilini
20.Taja madini 5 ambayo hupatikana kwenye maji
21.Kwanini tunashauriwa kuwapoa watoto vyakula
vyenye virutuibisho vya kutosha?
22.Wototo wadogo wanatakiwa kula vyakula vyenye
23.Taja vyakula 6 ambavyo tunasghauriwa kuwapa
watoto wadogo
24.Chakula kikuu cha watoto ni chakula chenye
virutubisho gani?
25.Taja umuhimu wa maziwa kwa watoto
26.Ili kusaida mtoto kuimarisha nguvu ya mwili wake
tunashauriwa kumpa vyakula gani?
27.Kijana anashauriwa kula vyakula vya aina gani
28.Orodhesha vyakula anavyo shauriwa kula kijana
29.Watu wanaofanya kazi nyepesi wanashauriwa
kufanya kazi gani?
30.Watu wanaofanya kazi nyepesi wnashauriwa kula
vyakula vyenye kiwango kidogo cha kabohaidreti
kwasababu gani
31.Watu wanaofanya kazi nyepesi wanashauriwa kula
vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nini?

32.Ulaji wa mbogamboga na matumnda husaidia nini
mwilini?
33.Kwanini wa mama wajawazito wanahitaji kula ml
kamili wenye virutubisho vya kutosha ………..
34.Chakula gani kinaweza kusaidia ukuaji mzuri wa
mtoto akiwa tumboni kwa mama yake…..
35.Vitu gani humsaidia mama mjamzito kuwa na damu
ya kutosha…..
36.Taja athari zinazoweza kumpata mtoto endapo
mama mjamzito hatapata mlo kamili wenye
vitubisho vya kutosha A]…..B…..C…..D…
37.Kwanini wagonjwa wanahitajika kula mlo kamili
wenye virutubisho A….B….C….
38.Wagonjwa wanahitajika kula vyakula vyenye kiasi
kikubwa cha vyakula gani? A….B…C…D..
39.Wagonjwa wanashauriwa kula vyakula vyenye kiasi
kikubwa cha protini,vitamin,madini ili kumsaidia
kufanya nini?
40.Ulaji wa mlo kamili unazingatia kitu gani?
41.Mtu mwenye ugonjwa wa anemia anashauriwa kula
vyakula gani?
42.Mtu mwenye shindikizo la juu la damu hapaswi kula
vyakula gani?
Na ni kwasababu gani?
43.Mtu mwenye shindikizo la juu la damu hapaswi kula
vyakula vyakula gani? A……B……C…..D….
44.Mtu mwenye shindikizo la chini la damu hapaswi
kula vyakula aina gani?
45.Wazee wanatakiwa kula vyakula gani?.....na
nikwasababu gani?
46.Kwanini wazee wanashauriwa kula vyakula vyenye
madini?
47.Wazee wanapaswa kula vyakla gani ili kuutia mwili
nguvu ?
48.Kwanini wazee wanashauriwa kula vyakula vyenye
protini?
MADA MFUMO WA FAHAMU
1.Nini maana ya mfumo wa fahamu?
2.Mfumo wa fahamu umegawanyika katika sehemu
kuu ngapi?
3.Taja muundo wa mfumo wa fahamu A…..B….
4.Mfumo wa fahamu wa kati umeundwa na nini?
5.Mfumo wa fahamu wa pembezoni umeundwa na
nini?
6.Chora mchoro kuonesha mfumo wa fahamu wa
binadamu
7.Ubongo ni sehemu gani ya mfumo wa fahamu?
8.Ubongo umegawanyika katika sehemu kuu ngapi?
9.Taja aina za ubongo A…B…C…
10.Ubongo wa binadamu unakadiriwa kuwa na kg
ngapi?
11.Taja sifa za ubongo wa serebram A……B….C…..D….
12.Orodhesha kazi za ubongo wa serebramu A…….B……
C….D…..
13.Ubongo wa serebramu huratibu matendo gani? A……
B……C…..D…..E…..F….G….H…..I….J….
14.Taja sifa za ubongo wa serebelamu……
15.Kubainisha kazi za ubongo wa serebelamu A……
B….C…D…..
16.Serebelamu huhusika na kuratibu matendo gani?
17.Kutaja matendo yanayo ratibiwa na ubongo wa
serebelamu? A….B….C….
18.Matendo ya hiari ni matendo gani?..
19.Kutaja mfano wa matendo ya hiari A…..B…..C…..D……
20.Kubainisha tofauti kati ya ubongo wa serebelamu na
serebram
21.Kubainisha sifa za ubongo wa medula oblongata
A……B…….C…….D…..
22.Medula oblongata huhusika kuratibu matendo gani?
23.Kuorodhesha matendo yanayoratibiwa na ubongo
wa medulla oblongata A….B….C…..D..
24. Matendo yasiyo ya hiari nini?
25.Taja mfano wa matendo yasiyo ya hiari A……B….C…
D……
26.Bainisha tofauti kati ya medulla oblonga na
serebelamu……
27.Bainisha tofauti kati ya serebramu na medula
oblongata?
28.Ubongo una umuhimu gani?
29.Ugwemgongo ni sehemu ya mfumo …. Wa fahamu
30.Ugwemgongo unalindwa na nini?
31.Taja neva ambazo zinapatikana katika ugwemgongo
A….B…..
32.Taja kazi ya ungwe mgongo
33.Ungwemgongo kazi yake nini?
34.Kutaja mfano wa matendo ya kuratibiwa na
ugwemgongo A……B…….C….
35.Bainisha kazi za mfumo wa kati wa fahamu…
36.Mfumo wa fahamu wa pembezoni huundwa na nini?
37.Neva nini?
38.Bainisha kazi za neva mwilini A……B……C…..D….
39.Kazi ya neva ni kuunganisha nini katika mwili
40.Neva ni miongoni mwa …..za mwili
41.Neva zimeundwa na nini?
42.Kila nyuroni katika neva ina nyukilias iliyozaa
43.Nyuklias na saitoplazimu huunda nini?
44.Saitoplazimu imeundwa nanini?
45.Bainisha kazi ya dendrait…..

46.Chora mchoro kuonesha ugwemgongo
47.Chora mchoro kuonesha muundo wa neva
48.Bainisha sifa za neva A….B…
49.Umbo la neva husaidia kufanya nini?
50.Bainisha sifa za neva sayatiki……
51.Bainisha tofauti kati ya mfumo wa fahamu wa kati na
mfumo wa fahamu wa pembezoni au nje?
52.Kuna milango mingapi ya fahamu?
53.Bainisha uusiano uliopo kati ya milango ya fahamu
na mfumo wa fahamu?
54.Ainisha milango mitano ya fahamu
55.Milango ya fahamu imeunganishwa na ubongo
kupitia kwenye nini?
56.Milango ya fahamu huchukua na kupeleka taarifa
kwenye ubongo kupitia kwenye nini?
57.Kwanini milango ya fahamu ni muhimu?
58.Jicho ni ogani inayojihusisha na kiamshi gani?
59.Neva katika jicho inayopeleka taarifa kwenye ubongo
huitwa?
60.Jicho hushikiliwa na nini?
61.Jicho limeundwa na sehemu ngapi?
62.Bainisha sehemu kuu za jicho
63.Bainisha sehemu za nje za jichoA….B….C…D…
64.Taja sehemu za ndani za jicho
a…..b…..c…..d…..e…..f….g…..h…..i….j….k….l….m….o….
p…q….
65.Taja kazi za
a.kifuniko cha jicho..
b.konjaktiva
c.konea
d.misuli ya siliari
e.lenzi
f.ute wa akwasi
g.irisi au mboni
h.pupili
i.ute wa vitrasi
j.retina
k.neva ya optiki
66.chora mchoro kuonesha sehemu za jicho
67.kuna aina ngapi za kasoro za jicho
68.orodhesha aina za kasoro za jicho
69.taswira katika jicho hufanyikia kwenye nini?
70.Taswira inayofanyikia kwenye jicho huwa katika hali
gani?
71.Taswira kitu katika jicho hutafsiriwa na nini?
72.Chora mchoro kuonesha taswira inavyoofanyika
kwenye jicho?